Skip to main content

Ukombozi wa watoto vitani wahitaji uwekezaji-Mwanaharakati

Ukombozi wa watoto vitani wahitaji uwekezaji-Mwanaharakati

Umoja wa Mataifa ukitathimini miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kitengo kinachohusika na ufuatiliaji wa masuala ya ukatili wa watoto vitani, mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Somalia Ilwad Elman, amesema ukombozi kwa watoto vitani unahitaji uwekezaji .

Ilwad ambaye alirejea nyumbani mwaka 2010 kutoka uhamishoni Canada na kuwa Mkurugenzi wa mipango na maendeleo katika taasisi iitwayo kituo cha amani na haki za binadamu cha Elman nchini Somalia, iliyoasisiwa na babaye aliyeuwawa kwa haratakati hizo miaka 20 iliyopita, anajihusisha na uragibishaji na ujumuishwaji wa watoto waliotumikishwa vitani.

Ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa usaidizi wa watoto vitani unahitaji ushirikiano wa jumuiya ya kimataifa na mashinani na kubwa ni.

( Sauti Ilwad)

‘‘Uragibishaji, na kuwapatia elimu upya watoto ni uwekezaji wa muda mrefu, sio kazi ambayo waweza kupata matokeo haraka. Inahitaji zaidi ya mtu mmoja Hususani ni katika muendelezo wa machafuko. Nataka kuikumbusha jamii ya kimataifa kwamba ina wajibu wa kuwalinda wadau wao mashinani’’