Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani operesheni za kijeshi hospitalini CAR

UM walaani operesheni za kijeshi hospitalini CAR

Umoja wa Mataifa umelaani operesheni ya kijeshi katika hospitali  nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, iliosababisha vifo vya raia watatu na kujeruhi wengine 26 mjini Bangui.

Taarifa ya kaimu mratibu nchini CAR ambaye pia ni mwakilishi wa shirika la afya ulimwenguni WHO Dk Michel Yao, operesheni hiyo katika eneo jirani na  kikosi namba PK5 lilisababisha madhara kwa raia na wanajeshi kwahivyo ametaka kuheshimiwa kwa sheria za kimataifa za kibinadamu.

Amesema kufuatia tukio hilo,  vikosi vilivamia kwa makusudi eneo hilo vikiwa na dhamira ya kuua waliojeruhiwa. Amelaani hatua ya vikosi vyenye silaha kuingia kwenya eneo la kituo cha afya.

Dk Yao amesema haikubalikai kwa kikosi chenye silaha kuvamia hospitali na kuua wagonjwa na kutaka wadau wote kuheshimu maeneo ya vituo vya afya na kuhakikisha wahudumu wa afya wanawafikia wagonjwa na madawa.

Katika operesheni hiyo, nyumba ,shule na kanisa viliteketezwa.