Skip to main content

Kuna haja ya kuisaidia Iraq baada ya Daesh-Kubiš

Kuna haja ya kuisaidia Iraq baada ya Daesh-Kubiš

Wakati operesheni za kuukomboa mji wa Mosul Iraq zikiendelea , jumuiya ya kimataifa, imeombwa kujikita katika siku ambayo mji huo utakuwa huru kabisa kutoka mikononi mwa kundi la itikadi kali la ISILambalo pia hujulikana kama Daesh.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ján Kubiš akizungumza katika kikao cha baraza la usalama kuhusu Iraq na mapango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMI, amesisitiza kwamba nchi hiyo itaendelea kuhitaji msaada wa kimataifa wakati huo utakapowadia.

(SAUTI YA KUBIS)

“Baada ya Daesh Iraq itaendelea kuhitaji msaada muhimu kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na wadau wengine wa kikanda, upunguzaji wowote wa ghafla wa kujihusisha na Iraq au msaada utamaanisha kurejea makossa ya nyuma. Makosa ambayo yanaathari kubwa kwa usalama na utulivu wa zaidi ya miapaka ya Iraq”

Naye Rais wa baraza la usalama kwa mwezi huu balozi wa Ukraine kwenye Umoja wa Mataifa Volodymyr Yelchenko

(SAUTI YA YURIY YELCHENKO)

“Tumeelezea hofu yatu kuhusu hali tete ya kibinadamu inayoendelea kote Iraq hususani mndani na katika viunga vya Mosoul. Tumesisitiza haja ya kuongeza juhudi za upatanishi hasa kwa kushirikisha wanawake na asasi za kiraia na wadau wengine kusaidia mchakato huo. Zaidi ya hayo tunatambua haja ya kuendelea kuisaidia Iraq katika ujenzi wa miundombinu muhimu hasa Mosoul na tumezitaka nchi zote wanachama kufikiria  uwezekano wa kuisaidia katika suala hili”