Warundi walioswekwa DRC warejea nyumbani kwa hiari

Warundi walioswekwa DRC warejea nyumbani kwa hiari

Hatimaye operesheni ya kuwarejesha nyumbani kwa hiari raia 124 wa Burundi walioingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kinyume cha sheria zaidi ya mwaka mmoja uliopita imekamilika.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO umesema raia hao waliingia wakiwa na raia wengine wa Rwanda ambapo walikamatwa na kuswekwa ndani humo Bukavu.

Baada ya mazungumzo kati ya pande mbili hizo, ilikubaliwa warejeshwe nyumbani kwa mujibu wa sheria za kimataifa ambapo wengine 65 hawakukubali kurejea.

Walilakiwa mjini Kavimvira mpakani mwa Burundi na DRC ambapo Waziri wa sheria wa Burundi amesema kurejea kwao nyumbani kwa hiari ni kiashiria cha kuwepo kwa amani nchini humo, akitoa wito kwa raia wengine wa Burundi warejee nyumbani.