Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSOM yawatunuku maafisa kwa kazi nzuri

UNSOM yawatunuku maafisa kwa kazi nzuri

Maafisa wa polisi na jeshi wanane wametunukiwa medali na vyeti kwa kutambua mchango na huduma zao kama washauri kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia UNSOM.

Raisedon Zenenga, naibu mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Somalia akikabidhi medali hizo kwa maafisa kutoka Sweden, Finland, Nepal na Malawi ambao wamekuwa polisi na wanajeshi washauri kwenye taasisi ya utawala wa sheria na usalama ya UNSOM nchini Somalia ijulikanayo kama ((ROLSIG).

Maafisa hao wametumwa na nchi zao kufanya kazi na UNSOM kwa kipindi cha kati ya miezi minne na sita. Bwana Zenenga amewapongeza maafisa hao kwa kazi nzuri, kujituma na kuwa wazi hali ambayo imeusaidia mpango wa UNSOM kutimiza wajibu wake Somalia.