Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yaleta nuru kwa wenyeji kambi ya Nyarugusu, Tanzania

WFP yaleta nuru kwa wenyeji kambi ya Nyarugusu, Tanzania

Nchini Tanzania, shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limeanza kuwapatia wakimbizi  10,000 fedha taslimu ili kujinunulia chakula badala ya kutegemea chakula chote kupitia mgao. Mradi huo ni wa majaribio na umeanza mwezi uliopita wa Disemba ambapo WFP inasema imewezekana baada ya kupata mchango wa dola za kimarekani 385,000 kutoka Canada. Je nini kinafanyika? Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa  Mataifa nchini Tanzania, amezungumza kwa njia  ya simu na Said Johari, mkuu wa ofisi ya WFP huko Kasulu, mkoani Kigoma ambako wanasimamia kambi hiyo ya Nyarugusu waliko wanufaika wa mradi huo. Bwana Johari anaanza kwa kuelezea ni vigezo gani walitumia kuchagua wanufaika hao 10,000.