Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya watoto Deir Ez Zor Syria iko njia panda-UNICEF

Hali ya watoto Deir Ez Zor Syria iko njia panda-UNICEF

Watoto wanaoishi katika mji wa Deir Ez Zor nchini Syria wamekabiliwa na mashambulizi makali katika kipindi cha wiki iliyopita. Hii ni kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Mkurugenzi wa kanda hiyo wa Shirika la kuhudumia watoto UNICEF. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

UNICEF inasema kuongezaka kwa vurugu kunatishia maisha ya raia 93,000, wakiwemo watoto zaidi ya 40,000 ambao wamekosa misaada  ya kibinadamu kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Imeongeza kuwa urushaji wa makombora kiholela umesababisha vifo vya raia na kulazimisha wengine kubaki katika nyumba zao, bei za vyakula zimepanda  mara tano zaidi ya ilivyo katika mji mkuu, Damascus.

Pia kuna uhaba wa maji safi na familia zinalazimika kuteka maji kutoka mto Eufrates bila kutia tembe za kuyasafisha na kuwawfanya  watoto kuwa katika hatari ya magonjwa yanayotokana na maji.Tamara Kummer ni afisa mawasiliano wa kikanda wa UNICEF

(SAUTI YA TAMARA)

“Tunatoa wito kwa pande zote kwenye mzozo kucha kuzingira maeneo hayo na kuruhusu bila masharti wahudumu wa misaada ya kibinadamu kuwafikia watoto Deir ez zor  na maeneo mengine yanayozingirwa nchini humo, hakuna kinachohalalisha hali hiyo na madhila yanayowakabili watoto”