Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto zaidi ya 23,000 wa Sudan Kusini wako kambi za wakimbizi Ethiopia-UNHCR

Watoto zaidi ya 23,000 wa Sudan Kusini wako kambi za wakimbizi Ethiopia-UNHCR

Zaidi ya watoto 23,000 wasio na wazazi wao kutoka Sudan Kusini wako kwenye kambi za wakimbizi nchini Ethiopia limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Hivi sasa watoto hao wamewekwa katika uangalizi maalumu wakati UNHCR ikijaribu kuwasaka wazazi na familia zao. Baadhi ya watoto hao walitenganishwa na wazazi wao kutokana na vita na wengine walisafiri peke yao.

Ethiopia hivi sasa inahifadhi wakimbizi 340,000 wa Sudan Kusini wengi wakitoka jimbo la Jonglei na Upper Nile, na hapo wanapatiwa malazi, chakula, huduma za afya na usafi.

Kisut Gebre Egziabher ni afisa habari wa UNHCR Ethiopia

(SAUTI YA EGZIABHER)

“Tuna idadi kubwa ya watoto waliowasili peke yao, ama walitengana na wazazi au walezi wao wakati wa safari za ndege ama walikuja tu peke yao kutoka Sudan Kusini. Hivyo idadi yao ni kubwa na ndio maana tumekuwa tukitoa wito wa dharura kwa watoto.”