Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuchaguliwa spika wa bunge Somalia ni hatua muhimu- AMISOM

Kuchaguliwa spika wa bunge Somalia ni hatua muhimu- AMISOM

Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM umelipongeza Bunge la watu nchini humo kufuatia uchgauzi wa spika wa chombo hicho hapo jana.

Kupitia wavuti wake, AMISOM imemnukuu Kaimu Mwakilishi maalum wa Mwenyekiti wa AU katika AMISOM Lydia Wanyoto, akiwapongeza wabunge kwa uchaguzi huo na kuahidi usaidizi wa ujumbe wake kwa Somalia ili kukamilisha mchakato wa uchaguzi.

Uchaguzi huo uliofanyika kwa utulivu umewezesha kupatikana kwa Spika, Naibu Spika wa kwanza na Naibu Spika wa pili.

AMISOM imesema hatua hiyo ni dalili njema za kuelekea kukamilisha mchakato wa uchaguzi nchini Somalia na kupongeza taifa hilo ambalo limeshudia vita kwa karibu miongo miwili kwa hatua hiyo ya kidemokrasia.