Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka saba baada ya tetemeko Haiti, UM waahidi mshikamano zaidi

Miaka saba baada ya tetemeko Haiti, UM waahidi mshikamano zaidi

Leo ikiwa ni miaka saba tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini Haiti lililosababisha vifo vya watu zaidi ya Laki mbili na zaidi ya milioni moja kukosa makazi, Umoja wa Mataifa umesema Haiti imeimarika zaidi na chombo hicho kitaendelea kuunga mkono taifa hilo.

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Haiti David Nabarro, amesema anatiwa moyo sasa kuwa Haiti imeimarika katika utulivu wa kisiasa kufuatia uchaguzi wa Rais na wabunge wa hivi karibuni.

Huko Haiti, wakati wa kumbukizi kwenye mji mkuu Port au Prince, tuzo za heshima zilizotolewa kwa mashirika na watu waliojitolewa kukwamua Haiti wakati na baada ya tetemeko hilo.

Miongoni mwa waliopatiwa tuzo hizo ni Umoja wa Mataifa ambapo mkuu wa ujumbe wake nchini Haiti, MINUSTAH, Sandra Honore alipokea kwa niaba akisema..

(Sauti ya Sandra)

“Nakubali heshima hii na tuko pamoja nanyi kifikra kukumbuka wananchi 230,000 wa Haiti ambao walifariki dunia wakati wa tukio hili.”