Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya uzazi ni msingi wa kuepuka VVU na Ukimwi

Afya ya uzazi ni msingi wa kuepuka VVU na Ukimwi

Afya ya uzazi kwa watoto wa kike na wasichana barubaru ni msingi wa kundi hili kuweza kujichanua na kufikia kiwango cha juu zaidi cha elimu. Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa usawa wa kijinsia ambalo ni lengo namba 5 la ajenda 2030 ya maendeleo endelevu linaweza kufanikiwa iwapo huduma ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike itapatikana bila vikwazo vyovyote.

Wasichana wanaweza kuepuka ujauzito katika umri mdogo, na hivyo kuwa na fursa ya elimu. Halikadhalika wanapofikia umri wa kuweza kuolewa, wanaweza kupanga uzazi na kupata fursa za kushiriki shughuli za kijamii na kiuchumi. Ili kufahamu harakati za Umoja wa Mataifa huko Cote d’Ivoire za kufanikisha huduma hiyo sambamba na madhila ya watoto wa kike, Amina Hassan amejikita kwenye makala hii.