Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misri yasaini mkopo wa dola bilioni moja, Benki ya Dunia

Misri yasaini mkopo wa dola bilioni moja, Benki ya Dunia

Benki ya Dunia na serikali ya Misri wametia saini mkataba wa mkopo wa dola bilioni moja, kwa ajili ya kuwezesha utekelezwaji wa miradi ya ukuaji jumuishi katika sekta muhimu za uchumi nchini humo. John Kibeog na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Kibego)

Kufuatia hatua hiyo, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Misri ambaye pia ni mwakilishi wa Misri kwenye Bodi ya Magavana wa Benki hiyo, Dkt. Sahar Nasr, ameonyesha matumaini kuwa msaada huo utawezesha serikali ya Misri kujitahidi kikamilifu na kuinua mtindo wa maisha kwa wananchi wote.

Amesema watafanikiwa kwa kuweka mazingira ya kiuchumi yanayotuliza mapato ya nchi, kuhakikisha usalama wa nishati, ufanisi, uwekezaji na kuboresha mazingira ya biashara ndogondogo na zile za kiwango cha kati.

Naye Asad Alam, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia anayehusika na Misri, Yemen Na Djibouti, amesema wanafurahia kuendelea kusaidia mradi kabambe wa Misri, unaotilia maanani upatikanaji wa ajira katika sekta binafsi na kuandaa mazingira ya ukuaji jumuishi.