Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Somalia wachukua hatua dhidi ya ukatili wa kijinsia

Vijana Somalia wachukua hatua dhidi ya ukatili wa kijinsia

Nchini Somalia vijana wameazimia kushirikiana na serikali ili kukabiliana na ukatili wa kijinsia ambao umeshamiri nchini humo.

Wametoa ahadi hiyo wakati wa kongamano lililofanyika kwenye mji mkuu Mogadishu kwa lenog la kubadilishana mawazo, ambao wamesema kuwa ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike  bado ni changamoto kubwa na juhudi zinahitajiki ili kuutokomeza.

Hassan Sheikh Mohamud ambaye ni mmoja wa washiriki wa kongamano hilo lililoandaliwa kwa pamoja na ujumbe wa muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, amesema ni muhimu pia ulinzi na usalama vikaimarishwa ili iwe rahisi kwa vijana kufika maeneo yote na kupazia sauti tatizo hilo.

Kongamano hilo ni sehemu ya kampeni inayolenga kupatia mafunzo vijana 300 katika wilaya zote 17 za Mogadishu kuhusu haki za binadamu na hivyo kusaidia kupunguza mizozano nchini Somalia.