Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna nchi iliyo salama dhidi ya ugaidi

Hakuna nchi iliyo salama dhidi ya ugaidi

Vikundi vya kigaidi vinatumia aina zote mpya za mitandao ya kijamii na teknolojia ya mawasiliano ili kupanua wigo wa mitandao yao sambamba na kufadhili shughuli zao.

Hiyo ni kwa mujibu mwakilishi wa kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi, Delphine Schantz alipohojiwa na chombo cha habari cha umoja huo.

Amesema tovuti na majukwaa mbali mbali kwenye mitandao hiyo inatumika kuchangisha fedha na kununua silaha kupitia kwenye mitandao akisema juhudi za pamoja zahitajika kufuatilia mifumo hiyo kwa kuwa..

(Sauti ya Delphine)

“Hakuna nchi mwanachama ambayo ni salama dhidi ya ugaidi au salama dhidi ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya ugaidi. Mfumo huu unafuatiliwa kwa karibu na nchi wanachama.”

Bi. Schantz amesema kamati yao hivi sasa inafuatilia tovuti zinazohusika na uandikishaji magaidi na uchangishaji fedha lakini jambo muhimu ni..

(Sauti ya Delphine-2)

“Ni kuhakikisha kuwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wana uelewa wa kutosha kuwa mitandao hii inaweza kutumika vibaya kueneza ujumbe mbaya wa kuchangisha fedha kwa ajili ya ugaidi na hivyo kuendeleza ubia kati ya sekta ya umma na binafsi ambao ni muhimu kupunguza hatari.”