Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

AMISOM kurejesha serikalini chuo chake cha Taifa Somalia

AMISOM kurejesha serikalini chuo chake cha Taifa Somalia

Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM uko mbioni kukamilisha mipango ya kukabidhi Chuo Kikuu cha Taifa cha Somalia kwa serikali ya nchi hiyo.

Katika taarifa yake AMISOM imesema hadi hivi karibuni chuo hicho kilikuwa chini ya uongozi wake kwa zaidi ya nusu muongo, kikitumiwa na jeshi la Burundi kama makao yake makuu.

Makubaliano ya kukabidhi chuo hicho yalifikiwa hivi karibu baada ya maamuzi ya kuhamishia kikosi cha Burundi Johwar kufikiwa.

AMISOM imesema itahakikisha inarejesha jengo hilo katika hali nzuri, baada ya jeshi lake kumaliza shughuli za kukikarabati.