Ban atuma salamu za rambirambi kufuatia shambulio la ugaidi Ujerumani

20 Disemba 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametuma salamu za rambirambi kufutia vifo vya watu 12 baada ya shambuliolinalodaiwa kuwa la kigaidi mjini Berlin Ujerumani

Polisi mjini humo wanasema ajali ya lori lililoacha njia na kuvamia soko maarufu kwa maandalizi ya krisimasi ilikuwa ya makusudi .

Taarifa ya msemaji wa Ban, imemnukuu Katibu Mkuu akizipa pole familia zilizopoteza wapendwa wao katika tukio hilo, serikali na watu wa Ujerumani pamoja na kuwatakia majeruhi uponyaji.

Amesema ana amatumaini kuwa yeyote aliyehusika katika kupanga ajali hiyo atafikishwa katika mkono wa sheria haraka.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter