Ban alaani mauaji ya mlinda amani wa UM nchini DRC

19 Disemba 2016

Imebainika kuwa mlinda amani aliyeuawa Jumatatu asubuhi huko Butembo, jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni kutoka Afrika Kusini.

Kufuatia taarifa hizo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani mauaji hayo yaliyofanyika wakati wa makabiliano kati ya askari wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa DRC, MONUSCO na wapiganaji wanaosadikiwa kuwa wa Mai-Mai.

Katika makabiliano hayo walinda amani wengine wawili wa Afrika Kusini walijeruhiwa.

Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mlinda amani huyo pamoja na serikali ya Afrika Kusini.

Amewatakia ahueni ya haraka majeruhi huku akitoa wito kwa serikali ya DRC kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa wa shambulio hilo.

Amesema mashambulizi dhidi ya walinda amani hayakubaliki kwa misingi yoyote ile.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter