Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani wa UM auawa DRC

Mlinda amani wa UM auawa DRC

Shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa Maï-Maï asubuhi ya leo huko Butembo jimbo la Kivu Kaskazini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC limesababisha vifo vya watu saba miongoni mwao mlinda amani mmoja wa Umoja wa Mataifa na polisi wa DRC. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Habari zinasema wapiganaji hao wa Mai Mai walijaribu kushambulia ukumbi wa jiji, ofisi za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, makao makuu ya polisi na gereza kuu la mji wa Butembo.

Hata hivyo jeshi la MONUSCO lilijibu mashambulizi ambapo waasi watano waliuawa.

Msemaji wa MONUSCO Félix Basse amewatoa hofu wakazi wa Kivu Kaskazini akisema dhamira na azma ya vikosi vilivyo kwenye operesheni iko juu na hivyo akatoa wito....

(Sauti ya Felix)

“Mosi wasijihusishe na vikundi hivyo vilivyojihami na pili watoe usaidizi na ushirikiano kwa vikosi vya ulinzi vya serikali vinavyoendesha operesheni zao kwenye eneo hilo na tatu kuhamasisha jamii ambayo wakati mwingine inakuwa ndiyo chanzo cha tatizo.”