Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuko kwa ajili ya raia wa Somalia-AMISOM

Tuko kwa ajili ya raia wa Somalia-AMISOM

Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, umewahakikishia wananchi nchini humo kuhusu ahadi ya kufanya kazi na mamlaka katika kuwapatia ulinzi raia .

Rosemary Musumba na taarifa kamili.

( TAARIFA YA ROSEMARY)

Ufafanuzi wa AMISOM uliochapishwa katika mtandao wa Twitter wa ujumbe huo , unafuatia kile ilichokiita tukio la bahati mbaya ambapo raia walipoteza maisha katika shambulio.

Ujumbe huo umesisitiza kuwa unasikitishwa na shambulio hilo lililotekelezwa na vikosi vyake katika operesheni za ulinzi wa amani eneo liitwalo Qorooley.

AMISOM inachunguza tuhuma dhidi ya vikosi vyake na kukusanya taarifa zaidi kabla ya kutoa tamko muhimu’’ imesema sehemu ya chapisho hilo.