Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko ECOWAS kwa msimamo wenu kuhusu uchaguzi Gambia- Ban

Heko ECOWAS kwa msimamo wenu kuhusu uchaguzi Gambia- Ban

Bendera ya Gambia.([Picha:UM/Loey Felipe)[/caption]Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza msimamo thabiti wa jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS kuhusu Gambia ambao pamoja na mambo mengine ni kuchukua hatua zozote za lazima kuheshimu matokeo ya uchaguzi wa Rais nchini Gambia ambapo mshindi alikuwa Adama Barrow.

ECOWAS ilisema itahakikisha ulinzi wa Rais mteule Barrow na kwamba jumuiya hiyo itashiriki sherehe za kuapishwa kwake tarehe 19 mwezi ujao.

Ingawa hivyo, Ban kupitia msemaji wake ameeleza wasiwasi wake kuhusu hali ilivyo nchini Gambia hivi sasa kufuatia uchaguzi uliofanyika tarehe mosi mwezi huu, hususan kitendo cha tume huru ya uchaguzi nchini humo kuendelea kuzingira na vikosi vya jeshi.

Amesihi jeshi la Gambia kuzingatia maadili yake ya kutopendelea upande wowote na kujizuia kuchukua hatua katika mazingira yoyote yatakayoibuka.

Ban amesema Umoja wa Mataifa kwa upande wake unaendelea kuunga mkono uamuzi wa ECOWAS na upo tayari kusaidia usuluhishi iwapo utaombwa kufanya hivyo kupitia Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na John Dramani Mahama wa Ghana.