Wanawake wana ufunguo wa kutokomeza njaa duniani- FAO

16 Disemba 2016

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema usawa wa kijinsia siyo tu ni jambo jema kimaadili bali pia ni muhimu katika kutokomeza njaa, ufukara na utapiamlo, amesema Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva huko Roma, Italia.

Akifungua mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kuwawezesha wanawake wa kijijini, da Silva amesema wanawake ni uti wa mgongo wa sekta ya kilimo na hivyo wapatiwe fursa ili mchango wao uwe endelevu.

Naye Kostas Stamoulis, Mkurugenzi msaidizi kutoka FAO amezungumzia mradi wao na UNHCR wa kuwapatia wanawake wa vijiini jiko bora ili kupunguza muda wa kupika akisema limewezesha..

(Sauti ya Kostas)

Ubora wa mapishi hii ikimaanisha lishe na afya bora na muda wa kuangalia watoto ni kutokana na jiko rahisi ambalo lilisambazwa kwa wanawake.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter