Skip to main content

Keating alaani vikali shambulio la kigaidi Mogadishu

Keating alaani vikali shambulio la kigaidi Mogadishu

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating amelaani vikali shambulio la kigaini la Jumapili nje kidogo ya bandari ya Somalia mjini Moghadishu ambapo asilimia kubwa ya wahanga ni raia.

Kundi la Al-Shabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo ambalo limeshanyika kwa kutumia lori lililosheheni mabomu na likatokea na kulipuka karibu na ofisi ya ushuru wa forodha. Msemaji wa kundi hilo ametanabaisha kuwa walikuwa wakiwalenga wafanyakazi wa usalama waliopangiwa kazi bandarini kwa sababu wanamafunzo ya kutoa usalama wakati wa uchaguzi.

Bwana Keating amesema shambulio hilo lililofanyika wakati wa mapumziko ya sherehe za kidini ni ushahidi mpya wa kundi hilo kutojali maisha na matumaini ya raia wa Somalia.