Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kimataifa dhidi ya ugaidi waimarishwa

Ushirikiano wa kimataifa dhidi ya ugaidi waimarishwa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kuhusu vitisho vya amani na usalama ulimwenguni likiangazia ushirikiano wa kimahakama kama njia ya kukabiliana na ugaidi.

Kikao hicho kilianza kwa wajumbe kupitisha kwa kauli moja azimio la kwanza kabisa la aina yake namba 2322 ambalo pamoja na mambo mengine linatoa wito kwa nchi wanachama kutathmini upya masuala ya kukabidhiana wahalifu na usaidizi wa pamoja wa kisheria kuhusu masuala ya kigaidi.

Akihutubia hadhira hiyo baada ya kupitishwa kwa azimio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa kamati tendaji ya Umoja wa Mataifa dhidi ya ugaidi Jean-Paul Laborde amesema…

(Sauti ya Laborde)

“Aina hii ya ushirikiano na udau baina ya taasisi za kimahakama unaimarisha uwezo wa serikali kuu kusaidia waendesha mashtakana na wapelelezi kwenye jitihada zao za kuhakikisha wanakuwa na taarifa za kimahakama kwa njia na wakati muafaka.”

Naye Dorcas Agik Oduor Naibu Mkurugenzi kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka nchini Kenya amesema kwa sasa mashtaka dhidi ya watuhumi wa ugaidi yanaendeshwa na watendaji ambao bado stadi kwenye sekta hiyo ni changamoto hivyo amesema…

 (Sauti ya Dorcas)

“Kuchagiza muingiliano wa sheria za kitaifa ili kuanzisha marekebisho ya kina ya kanuni na pia na kuanzisha kwa ujumla uwezo mpana zaidi wa kuchunguza na kufungua mashtaka katika ngazi ya taifa na pia kuimarisha uwezo wa ushirikiano katika ngazi ya kimataifa.”