Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wenye HIV hukabiliwa na ubaguzi kuliko wanaume

Wanawake wenye HIV hukabiliwa na ubaguzi kuliko wanaume

Kuelekea siku ya Ukimwi duniani hapo kesho Disemba mosi, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Ukimwi UNAIDS limeandaa tukio maalum leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa lenye maudhui kusonga mbele pamoja, asiachwe mtu nyuma.

Wakati hayo yakijiri, msichana kutoka India, mwenye virusi vya Ukimwi ameimbia redio ya Umoja wa Mataifa kuwa wanawake wenye virusi wanakabiliwa na ubaguzi zaidi ya wanaume.

Lalchhuanzuali anayewakilisha taasisi ya vijana iitwayo LEAD amekuja katika makao makuu ya UM kuzungumzia madhila yanayowakumba vijana waathirika wa HIV na anataja kwanini wanawake hukabiliwa na ubaguzi zaidi.

(SAUTI Lalchhuanzuali)

"Kwasababu ya ukosefu wa usawa wa kijinsia, kama msichana, pale watu wanapofahamu nina HIV wanauliza umepata wapi virusi? Lakini kwa wanaume hawahoji swali hilo. Wananichukulia kama malaya , ndiyo maana nimeambukizwa.’’