Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu anastahili huduma na ulinzi dhidi ya Ukimwi: Ban

Kila mtu anastahili huduma na ulinzi dhidi ya Ukimwi: Ban

Kwaya maalum ikihamasisha kuhusu makabiliano dhidi ya ukimwi katika tukio maalum hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Katika hotuba yake wakati wa tukio hilo la siku ya ukimwi duniani ambayo itaadhimishwa kesho Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema makabiliano dhidi ya ukimwi ni muhimu kwa kuwa kila mtu anastahili matibabu na makundi hatarishi yote yanastahili ulinzi dhidi ya unyanyapaa na ukatili.

Ban amewaambai wadau mbalimbali walikousanyika katika makao makuu ya umoja huo mjini New York kuwa ili kufikia malengo ya watu milioni 30 kupatiwa tiba ifikapo mwaka 2030 kinahotajika ni.

( SAUTI BAN)

‘Tuyafikie makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, wasichana katika ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara, watu wanaojidunga sindano, wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na masikini wanaohitaji huduma na matibabu.’’