Ukatili na ubaguzi dhidi ya LGBT utokomezwe: UM
Hatua tano muhimu zinahitajika ili kukomesha ukatili na ubaguzi dhidi ya jamii ya watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na waliobadili jinsia au LGBT, kote duniani.
Wito huo umetolewa na mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa kimataifa kuhusu LGBT unaofanyika nchini Thailand. Hatua hizo kwa mujibu wa Vitit Muntarbhorn ni pamoja na kuondoa sheria zinazowaathiri wasagaji, mashoga, wanaofanya mapenzi na watu wa jinsia zote mbili na waliobadili jinsia (LGBT), na kutowaona watu wa jamii inayosumbuliwa na ugonjwa.
Ametaja hatua zingine kuwa ni kuwapa watu hawa haki ya jinsia zao kutambuliwa katika nyaraka rasmi, kushirikiana na tamaduni tofauti na dini ili kuhakikisha wanajumuishwa na kuhakikisha watoto wanakuwa na hulka ya kuthamini na kuheshimu watu wa jinsia tofauti na mwelekeo tofauti wa kimapenzi.