Shambulio la kigaidi lililoua 32 Afghanistan limelaaniwa na UM

21 Novemba 2016

habariunamaShambulio la kigaidi nchini Afghanistan lililokatili maiasha ya raia 32 mjini Kabul, limelaaniwa vikali na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyekluwa amevaa vifaa vya mlipuko amejilipua kwenye msikini wa Baqer-ul Jumatatu ambako waumini Kiislam wa Kishia walikuwa wamekusanyika kuadhimisha arbadeen sherehe za siku ya 40 baada ya Ashura.

Wengi wa waliopoteza maisha ni watoto, huku watu wengine 50 wakijeruhiwa. Akizungumza kutoka mjini Kabul naibu mkuu wa UNAMA , Pernille Kardel, ameelezea shambulio hilo kama ni “ukatili”.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter