Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatutakomesha ukatili dhidi ya wanawake ikiwa kuna ukosefu wa fedha

Hatutakomesha ukatili dhidi ya wanawake ikiwa kuna ukosefu wa fedha

Leo hapa makao makuu kunafanyika mkutano rasmi wa kuadhimisha siku ya kimataifa wa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake ambayo kwa kawaida huadhimishwa tarehe 25 Novemba kila mwaka, ambapo Umoja wa Mataifa unasema harakati za kutok omeza tatizo hili sugu linazoroteshwa na uhaba mkubwa wa ufadhili wa fedha.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye ameshiriki katika mkutano huo kwa mara ya mwisho kabla ya kumaliza uongozi wake mwishoni mwa mwaka huu amesema, anawashukuru wadau wote katika harakati za kutokomeza ukatili wa aina zote dhidi ya wanawake. Amesema bila rasilimali za kutosha, lengo hili ambalo ni lengo nambari tano la maendeleo endelevu halitafikiwa ifikapo mwaka 2030 na hivyo.

(Sauti ya Ban) 

" Natoa wito kwa serikali kuonyesha mshikamano wao kwa kuongeza kwa hali ya juu matumizi ya taifa katika maeneo husika, ikiwa ni pamoja na msaada katika harakati za wanawake na asasi za kiraia. Na pia natoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na Wanawake, UN Women na katika mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake".