Sudan Kusini msikate tamaa: Loj
Baraza la usalama leo limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu Sudan na Sudan Kusini, ripoti ya kipindi cha kuanzia Ugosti 12, 2015 hadi 25 Okotoba mwaka 2016.
Akilihutubia baraza hilo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Ellen Margrethe Loj mbaye pia ni mkuu wa ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS, amesema hali nchini humo bado ni mbaya licha ya juhudi za jumuiya ya kimataifa za upatanishi na kukomesha machafuko.
Bi Loj anayemaliza muda wake katika nafasi hiyo ameliasa taifa hilo mambo mawili.
( SAUTI LOJ)
‘‘Tofauti katia ya mafaniko na kushindwa kwa makubaliano ya amani na amani Sudan Kusini, utasalia kwenye ahadi za pande katika umuhimu wa utekelezaji jumuishi. Pili, nawataka wahusika wote hususani viongozi wa Sudan Kusini wasipoteze mwelekeo wa lengo kusudiwa, la amani na mustakabali mwema kwa watu wa Sudan Kusini.’’
Kwa upande wake Adama Deng ambaye ni mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari amesema baada ya kutembela Sudan Kusini hivi karibuni, hali ya kibinadamu hususani jimboni Yei ni mbaya na kwamba dalili za mauaji ya kimbari ziko wazi.
Amesema machafuko nchini humo yameanza kama ya kisiasa lakini yanaelekea kuwa ya kikabila na akataka wadau wachukue hatua kabla nchi hiyo haijatumbukia katika mauaji ya kimbari an uhalifu wa kivita wa kiwango cha juu.