Skip to main content

Haki na maridhiano ni muhimu katika mchakato wa amani CAR, Mtaalamu

Haki na maridhiano ni muhimu katika mchakato wa amani CAR, Mtaalamu

Wakati mkutano mkubwa wa wahisani kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ukisubiriwa kwa hamu kufanyika kesho huko Brussles, Ubelgiji, mMtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Marie-Thérèse Keita-Bocoum, amesema haki na maridhiano nchini humo ndio muarobaini wa kudumu. John Kibego na taarifa kamili

(Taarifa ya John Kibego)

Bi. Keita-Bocoum, amesema katika taarifa yake kuwa bila juhudi hizo za kimataifa, mikataba kadhaa iliyoridhiwa na CAR, haitakuwa na maana katika nchi hiyo iliyozongwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya hivi karibuni bila haki na maridhiano.

Amesema licha ya kupungua kwa mapigano yaliyohusisha wanamgambo wa kikristu wa Anti-Balaka, na waasi wa kiislamu wa Seleka mwaka 2013, kumeshuhudiwa mapigano makali katika miezi ya hivi karibuni.

Mtaalamu huyo huru amesisitiza kuwa, mpango wa taifa wa kujenga amani, CAR, ulioanzishwa na serikali katika ushirikiano na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia utapata mafanikio kulingana na ahadi zitakazotolewa kwenye mkutano huo wa kesho.