Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Milango ya ajira kwa albino yaanza kufunguka Kenya

Milango ya ajira kwa albino yaanza kufunguka Kenya

Mkutano wa siku mbili wa viongozi wa Afrika wenye ulemavu wa ngozi, au albino umemalizika nchini Kenya kwa kupitisha mpango kazi wa kikanda wa kupambana na mashambulizi na ubaguzi dhidi ya kundi hilo.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Akizungumza kwenye mkutano huo, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za albino, Ikponwosa Ero amesema mpango huo unahusisha ushiriki wa jamii kwenye ulinzi akisema tayari Malawi imeanza kwa kuimarisha milango na vitasa vya familia zenye albino.

Naye mbunge Isaac Mwaura kutoka Kenya ambaye naye ni mlemavu wa ngozi amegusia ajira akisema jamii inaelimika akitolea mfano jinsi shindano la ulimbwende Kenya lilivyoleta mafanikio.

(sauti ya Mwaura)

Mkutano huo ulileta washiriki kutoka nchi 15 wakiwa ni wawakilishi wa serikali, mashirika ya kiraia na taasisi za haki za binadamu.