Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko Trump, tunatarajia ushirikiano na Marekani uendelee- Ban

Heko Trump, tunatarajia ushirikiano na Marekani uendelee- Ban

Umoja wa Mataifa umempongeza Rais mteule wa Marekani, Donald Trump kwa kuchaguliwa kuongoza taifa hilo kwa kipindi cha miaka minne. Rosemary Musumba na ripoti kamili.

(Taarifa ya Rosemary)

Ndivyo alivyoanza tamko lake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon mbele ya wanahabari, asubuhi ya leo Jumatano akisema anampongeza Donald Trump kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani.

(Sauti ya Ban)

“Baada ya kampeni iliyokuwa na ushindani na mgawanyiko, ni vyema kukumbuka na kusisitiza kuwa umoja na utofauti nchini Marekani ni moja ya sifa kubwa chanya ya taifa hili. Nasihi wamarekani wote wasalie na moyo huu.”

Amesema changamoto za sasa zinahitaji udau wa pamoja na hivyo….

(Sauti ya Ban)

 “Umoja wa Mataifa unatarajia uongozi mpya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa wakati tunahangaika kuendeleza pamoja yanayotuhusu, kukabili mabadiliko ya tabianchi na kusongesha haki za binadamu ili kutekeleza malengo endelevu kwa ustawi na utu wa wote.”