Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COP22 yaanza leo Marrakesh, Morocco

COP22 yaanza leo Marrakesh, Morocco

Mkutano wa 22 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi umeanza huko Marrakesh, Morocco, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuanza kutekelezwa kwa mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Umoja wa Mataifa unasema mkutano wa Marrakesh ni hatua muhimu kwa serikali kuangalia jinsi ya kuweka kwenye utekelezaji mkataba wa Paris, kwa kuwa mkataba umeonyesha njia na sasa ni kusaka mwelekeo.

Nalo shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeangazia wakulima likisema mabadiliko ya tabianchi ni mwiba kwa kundi hilo, likionya kuwa takribani wakulima milioni 120 wanaweza kutumbukia kwenye umaskini iwapo hatua hazitachukuliwa kuwanusuru.

Rob Vos ni mkurugenzi wa maendeleo ya uchumi wa kilimo, FAO

(Sauti ya Vos)

“Kilimo tayari kinaathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na kubwa zaidi ukame, upungufu wa mvua ni kawaida. Inahisiwa kilimo pia kinaleta karibu asilimia 20% ya hewa chafuzi. Hali hii inabadilisha kilimo na kwamba biashara kama kawaida si chaguo kwa wakulima, kuna uharibifu na matumizi mabaya ya ardhi. Kuna haja ya kukarabati uwezo wa dunia kama upandaji miti na matumizi endelevu ya ardhi”.