Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa 9 wa kimataifa kuhusu afya kufanyika Shangai:WHO

Mkutano wa 9 wa kimataifa kuhusu afya kufanyika Shangai:WHO

Katika kuashiria hatua kubwa kwenye afya ya kimataifa, viongozi zaidi ya 1,000 katika siasa, afya na maendeleo watashiriki katika kwenye mkutano wa 9 wa Kimataifa wa kuchagiza afya katika mjini Shanghai kuanzia Novemba 21-24.

Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la afya ulimwenguni WHO na serikali ya Jamhuri ya China. Maudhui ya mkutano ni kutoa fursa ya kutanabaisha ni ni jinsi gani ilivyo muhimu kuchagiza uwezo wa watu wote kuweza kufikia kiwango cha afya kinachostahili kwa kuboresha usawa na maendeleo endelevu katika nchi zote.

Mkutano huo utakuwa wa kihistoria , kwani mwaka 2016 unaadhimisha miaka 30 tangu kufanyika kwa mkutano wa kwanza kabisa wa kimataifa kuchagiza afya ambao uliibuka na mkataba wa afya wa Ottawa lakini pia ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s