Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR kuongeza msaada wa fedha za kuwasajili wakimbizi ifikapo mwaka 2020

UNHCR kuongeza msaada wa fedha za kuwasajili wakimbizi ifikapo mwaka 2020

Shirika la Umoja wa Mataifa Shirika la kuhudumia wakimbizi, UNHCR hivi leo imetangaza nia ya kuongeza msaada wa fedha inazowapatia wakimbizi kote duniani ifikapo mwaka 2020 kama njia bora ya kuwasaidia na kulinda usalama wao. Filippo Grandi, Kamishna mkuu wa shirika hilo amesema matumizi ya msaada wa fedha kwa wakimbizi yameleta mabadiliko makubwa kwa maisha yao na hivyo kuamua kuitekeleza sera hiyo kote duniani.

Kamishna huyo mkuu ameongezea kuwa wakimbizi wanafahamu bora mahitaji yao na msaada wa kifedha unawawezesha kupanga bajeti za familia zao na pia kuishi maisha ya heshima. Msaada huo pia una faida kwa wafanyabiashara, kuinua uchumi na kuendeleza uhusiano kati ya wakimbizi na jamii wanakoishi.

UNHCR ni moja ya mashirika ya kwanza kwa Umoja wa Mataifa kuanzisha msaada wa fedha mnamo miaka ya themanini na imepata ujuzi kwa mradi huo.

Tayari UNHCR inatoa misaada ya fedha kwa nchi 60 na kumekuwa na mafanikio hasa nchini Jordan na Lebanon kwa wakimbizi wa Syria wanaotoka kwenye mazingira magumu.

UNHCR kuanzia mwaka wa 2017 wataanzisha mpango huo katika nchi 15 zaidi ikiwa ni pamoja na Niger, DR Congo, Kenya, Congo Brazzaville, Rwanda, Somalia, Sudan, Ethiopia, Uganda, Afghanistan na Iran hadi mwaka wa 2020.