Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ili kubadili dunia ni lazima kubadilisha miji-Ban

Ili kubadili dunia ni lazima kubadilisha miji-Ban

Ikiwa leo ni siku ya miji duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ili kubadili dunia ni lazima kubadilisha miji kwa kuendeleza ustawi wa kimataifa, amani na haki za binadamu. Rosemary Musumba na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA ROSE)

Katika ujumbe wake kwa siku hii, Ban amesema kwa kuzingatia kuwa nusu ya idadi ya watu duniani wanaishi mijini na idadi hiyo inatarajiwa kukuwa kwa theluthi mbili ifikapo mwaka 2050, nilazima kukabiliaan na changamoto kama vile uhalifu, uchafu wa mazingira, na umaiskini ambavyo vinazidi kuathiri wakazi wa mijini.

Amesema wakazi hao wanaathiriwa kwani maeneo mengi ya miji yanaendelea na matumizi ya nishati, uvumbuzi na mabadiliko ya kiuchumi. Katibu mkuu ameongezea kuwa mkutano wa hivi karibuni Habitat III umependekeza ajenda mpya kwa ajili ya miji salama na endelevu.