Skip to main content

ICC yawasilisha ripoti Baraza Kuu

ICC yawasilisha ripoti Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limesikiliza ripoti ya mwaka ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC. Ripoti hii inakuja wakati huu ambapo nchi tatu za Afrika zimejiondoa katika mahakama hiyo. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA YA AMINA)

Nchi ambazo zimejitoa ICC ni Burundi, Gambia na Afrika Kusini, ambapo katiak mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa kabla ya kuwasilisha ripoti hiyo, Rais wa ICC aliyewasilisha ripoti hii leo Silvia Fernadez de Gurmedi amezitaka nchi hizo zifikirie uamuzi huo.

Bi Silvia amesema maombi yanayoletwa kwenye mahakaman hiyo hayapouuzwi kamwe haijalishi yanatoka ukanda gani.

(SAUTI SILIVIA)

‘‘Sisi hatupuuzi maombi yote tunayoyapata kutoka nchi wanachama, nchi za Afrika zikiwemo na nchi zingine za kimataifa ili haki za wale wote waliofanyiwa maovu zichunguwe ili kuleta usawa wa kila mtu. Na juu ya kujiondoa kwa nchi hizo tunazidi kuwaomba wafikirie upya uwamuzi wao wa kujitoa.’’