Skip to main content

Watoto milioni 300 wanaishi kwenye uchafuzi mkubwa wa hewa:UNICEF

Watoto milioni 300 wanaishi kwenye uchafuzi mkubwa wa hewa:UNICEF

Takriban watoto milioni 300 , au mmoja kati ya saba kote duniani wanaishi kwenye maeneo yenye viwango vikubwa vya uchafuzi wa hewa nje utokanao na sumu , kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Uchafuzi wa hewa unahusishwa na matatizo ya homa ya mapafu namaradhi mengine ya kupumua ambayo huua watoto , au kuathiri maendeleo yao , na watoto masikini ndio waathirika zaidi.

Ripoti hiyo “safisha hewa kwa ajili ya watoto”imetolewa kabla ya kuanza kwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi au COP22 , utakaoanza wiki hii mjini Marrakech, Morocco.

Nicholas Rees, ni mtaalamu wa sera wa UNICEF katika masuala ya uchumi na tabia nchi, pia ni mwandishi wa ripoti hiyo

(SAUTI YA NICHOLAS REES)

"Tumeweza kupata idadi ya watoto wanaoishi katika maeneo ambayo uchafuzi wa hewa umepindukia viwango vya WHO na pia maeneo yaliyoathirika zaidi. Maeneo hayo ni Asia, Asia Mashariki, Mashariki ya Kati na Afrika."