Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC ichunguze hima mauaji ya watoto 22 na walimu sita Syria: Brown

ICC ichunguze hima mauaji ya watoto 22 na walimu sita Syria: Brown

Mauaji dhidi ya watoto 22 na walimu sita huko Idlib nchini Syria ni uhalifu wa kivita dhahiri mauaji hayo yanapaswa kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua na mahakama kimataifa ya uhalifu ICC.

Hayo ni kwa mujibu wa Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu Gordon Brown ambaye amezungumza na waandishi wa habari mjini New York hii leo.

Bwana Brown ambaye ameonyesha dhahiri kusononeshwa na tukio hilo amesema.

( SAUTI BROWN)

‘‘Hili nishambulio baya zaidi kwa watoto wa shule, miongoni mwa mashambulio tofauti 98 nchini Syria kwa kipindi cha miaka miwili. Nalitaka baraza la usalama likubali kuwa mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, afanye uchunguzi wa kile ninachoamini ni uhalifu wa kivita, kwa lengo kwamba ikiwa itaathibitika watakelezaji wasakwe na kesi dhidi yao ifikishwe mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu.’’

Mjumbe huyo wa elimu ameongeza kuwa hakuna sababu ya baraza la usalama kuchelewa kukutana kwani hata Urusi imeruhusu uchunguzi ufanyike haraka.

Mjumbe huyo pi ametangaza kuwa mfuko wa elimu unaojumisha mashirika ya Umoja wa Mataifa , benki ya dunia na taasisi nyingine umetenga kiasi cha dola milioni 52 kwa ajili ya elimu nchini Syria ambao unatarajiwa kuwasaidia watoto milioni na nusu wasio shuleni kutokan na kadhia za vita.