Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wa maendeleo wajumuishe wakimbizi wa ndani kwenye mipango: Kang

Wadau wa maendeleo wajumuishe wakimbizi wa ndani kwenye mipango: Kang

Mpango mpya wa kuawajumuisha wakimbizi wa ndani unahitaji serikali na wadau wa maendeleo kujumuisha wakimbizi wa ndani katika mipango yao amesema msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kibinadamu Kyung-wha Kang. Taarifa azaidi na Grace Kaneiya.

(TAARIFA YA GRACE)

Akizungumza wakati wa mkutano hapa makao makuu wenye dhima ya mikakati yenye ufanisi kwa wakimbizi wa ndani, Kang ambaye pia ni Naibu mratibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, amesema mfumo huo utasaidia wakimbizi wa ndani kupata mahitaji ya msingi kama nyumba na fursa za ustawi.

( SAUTI KANG)

‘‘Ina maana sisi wadau, lazima tuunge mkono na kusimamia utekelezaji wa sheria za mfumo malmaka za mitaa na kuhitaji wawekezaji wa wafadhili kutoa kwa kunyumbulika fedha za usaidizi’’

Amesema nchi kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo DRC na Colombia zimeanza kutekeleza mfumo mpya huo na kutaka nchi nyigine kuiga mfano.