UM waomba saa 72 zaidi za usitishaji uhasama Yemen: Cheikh

UM waomba saa 72 zaidi za usitishaji uhasama Yemen: Cheikh

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, amezitaka pande zote mbili za mzozo kukubaliana na kuongeza saa 72 zingine zaidi za usitishaji uhasama. Ombi hilo limetolewa baada ya saa 72 za hapo awali kumalizika hii leo.

Bwana Ahmed amesema saa 72 za awali zimewapa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine fursa kubwa ya kufikisha misaada ya kibinadamu hususan chakula kwa maeneo yalioathirika.

Amezikumbusha pande zote katika mzozo huo masharti ya usitishaji wa uhasama pamoja ili kuleta mazingira bora kwa ajili ya upatikanaji wa amani ya kudumu nchini humo.