Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia yahimizwa kupambana na ubakaji-UM

Liberia yahimizwa kupambana na ubakaji-UM

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inasema asilimia kubwa ya wanawake na wasichana nchini Liberia wanabakwa na wanaofanya ukatili huo hawafikishwi mbele ya sheria.Taarifa kamili na Flora Nducha.

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, visa hivyo ambavyo vinaendelea hadi sasa, ni pamoja na ubakaji uliofanyika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14 nchini Liberia, ambapo asilimia kati ya 61.4 na 77.4 ya wanawake na wasichana walibakwa, na tathmini ya hivi karibuni ya mwaka 2015 inayoonyesha kwamba wengine 803 wamebakwa. Marcel Akpovo ni Afisa wa Ofisi ya Haki za Binadamu nchini Liberia....

(Sauti ya Akpovo)

"Kumekuwa hakuna uwajibikaji kwa wahusika wa makosa ya jinai na uhalifu wa kivita nchini Liberia, ikiwa ni pamoja na wahusika wa ukatili wa kingono katika vita. Na pia hapajakuwa na uwajibikaji wa ubakaji wa hivi karibuni ambao pia tumeurekodi. Ni asilimia mbili tu ya visa hivyo ndizo vimetendewa haki kmahakamani . Waathirika hawapewi haki zao kutokana na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na udhaifu wa kitaasisi, rushwa, ukosefu wa bidii za serikali na vile vile vikwazo vya kiufundi na kifedha."