Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa haki za binadamu wa UM na serikali ya Burundi wajadili mustakhbali wa ushirika wao

Mkuu wa haki za binadamu wa UM na serikali ya Burundi wajadili mustakhbali wa ushirika wao

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein na balozi wa Burundi Geneva wamekutana kujadili mustakhbali wa ushirika wao kufuatia uamuzi wa serikali ya Burundi kusitisha aina yoyote ya ushirikiano na ofisi ya haki za binadamu.John Kibego na taarifa kamili

(TAARIFA YA KIBEGO)

Hatima ya shughuli za ofisi hiyo sasa iko mikononi mwa serikali ya Burundi ambayo baada ya majadiliano itatoa uamuzi .

Zeid amesema kwa takriban miaka 20 ofisi yake imekuwa ikitoa muongozo na usaidizi wa kuboresha taasisi za serikali katika kuchagiza na kulinda haki za binadamu. Ameitaka serikali kufikiria upya uamuzi wake. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASAN)

“Kamishina mkuu pia amesikitishwa na uamuzi wa serikali ya Burundi wa kutangaza kutowataka wataalamu huru watatu wa tume iliyoanzishwa na baraza la haki za binadamu kufanya uchunguzi huru wa Umoja wa Mataifa Burundi .”

Ameongeza kuwa Kamishina ameitaka serikali kuendelea kujihusisha na mifumo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.