Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustakhbali wa Burundi uko mikononi mwa Burundi: Benomar

Mustakhbali wa Burundi uko mikononi mwa Burundi: Benomar

Mustakhbali wa Burundi uko mikononi mwa Burundi yenyewe . Hiyo ni kauli ya mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu kuzuia migogoro , ikiwemo Burundi Jamal Benomar, ambaye ametoa taarifa Alhamisi kwenye baraza la usalama kuhusu utekelezaji wa azimio nambari 2303 la mwei Julai mwaka huu kuhusu Burundi.

Amesema Burundi imekataa mapendekezo ya azimio hilo na sasa anaelekea nchini humo kwa ajili ya majadiliano na serikali , ili kusikiliza msimamo wao na hofu yao, ikiwa ni pamoja na kuwaelezea mawazo na lengo la baraza la usalama. Amesema hali iliyoanza kama mtafaruku wa kisiasa unaweza kusuluhishwa tu kisiasa

(SAUTI YA BENOMAR )

“Warundi wamedhihirisha wenyewe muongo mmoja uliopita , walipoibuka kutoka vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoshuhudia maelfu ya watu wakiuawa na kutawanywa.”

Ameongeza kuwa kwa mantiki hiyo Burundi ana ufunguo wa mustakhbali wake

(SAUTI YA BENOMAR )

"Nina hakika kwamba kwa utashi wa kisiasa na uongozi, Burundi wanaweza kutafuta njia ya kutoka kwenye mgogoro huu kupitia mazungumzo na maelewano."