Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika Kusini yataka kusitishwa uovu nchini Libya

Afrika Kusini yataka kusitishwa uovu nchini Libya

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametoa wito wa kusitishwa kwa uovu unaoendelea nchini Libya pamoja na mashambulizi ya anga kutoka kwa vikosi vya jumuiya ya kujihami ya nchi na Magharibi NATO.

Zuma ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa muungano wa Afrika AU ulikuwa na mpango wa kutatua mzozo nchini Libya kwa amani lakini hata hivyo haukupata muda wa kufanya hivyo. Zuma ameongeza kuwa Afrika Kusini itashirikiana na Baraza la Kitaifa la mpito nchini Libya linapojaribu kubuni serikali ya mpito.

(SAUTI YA JACOB ZUMA)