FAO kuchangia uhakika wa chakula sahel kupitia usimamizi wa ndege maji:

FAO kuchangia uhakika wa chakula sahel kupitia usimamizi wa ndege maji:

Shirika la chakula na kilimo FAO na kituo cha kimataifa cha mazingira cha Ufaransa (FFEM) watashirikiana katika ubiya mpya ili kuboresha hali ya maliasili katika ardhi oevu kanda ya Sahel barani Afrika, na hasa usimamizi endelevu wa ndege maji wanaohama ambao ni muhimu kwa uhakika wa chakula kwa wakazi wa eneo hilo.

Mkataba uliotiwa saini leo baina ya FAO na FFEM ambao utafadhili theluthi ya Euro milioni tano zinazohitajika katika mradi huo, utalenga nchi nne zenye ardhi oevu sahel ambazo ni Chad, Misri, Mali, Senegal na Sudan.

Katika nchi hizo miradi itajikita kwenye kuimarisha utaalamu udhibiti na matumizi kwenye bonde la mto Senegal, Niger Delta, ziwa Chad na mto Nile.

Maeneo hayo yamechaguliwa kwa sababu ni muhimu sana kwa uhakika wa chakula wa watu takribani bilioni moja ambao wanategemea kilimo, ufugaji na matumizi ya mali asili kama uvuvi na uwindaji wa ndege.