Skip to main content

Baraza la usalama, lajadili uchaguzi Somalia

Baraza la usalama, lajadili uchaguzi Somalia

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekutana kwa ajili ya mashauriano kuhusu Somalia likiangazia mchakato wa uchaguzi katika taifa hilo la pembe ya Afrika ambalo limeshushudia machafuko kwa takribani miongo miwili.

Flora Nducha na taarifa kamili.

( TAARIF YA FLORA)

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating ameliambia baraza kuwa mchakato wa uchaguzi ni mgumu ambao haukwepeki licha ya ugumu huo.

Amesema changamoto kadhaa zinaendelea kulikabili taifa hilo zikiwamo usalama, hali mbaya ya kibinadamu , ukosefu wa chakula, haki za binadamu husuani madhila kwa wanawake na watoto.

Keating amesema licha ya changamoto hizo kubwa zaidi ikiwa mgawanyiko wa jamii za Somalia, bado kuna matumaini ya kuleta mabadiliko kupitia uchaguzi huo wa kihistoria mapema mwezi ujao hivyo akatoa msimamo.

( SAUTI KEATING)

‘‘Tumedhamiria kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unatekelezwa, tukiwa tunaelewa vyema changamoto hizo. Hakuna kuchelewa tena, na tunaelewa athari ikiwa uchaguzi hautakuwa halali na mkamilifu.’’