Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jopo huru lichunguze mauaji ya wamarekani weusi- Wataalamu

Jopo huru lichunguze mauaji ya wamarekani weusi- Wataalamu

Jopo la wataalamu wa haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limetaka kufanyika uchunguzi huru dhidi ya mauaji ya wamarekani weusi yanayofanywa kinyume cha sheria na polisi huko Marekani.

Wataalamu hao wanaojikita katika watu wenye asili ya Afrika wametoa wito huo kufuatia mauaji ya Keith Scott huko jimbo la Carolina Kaskazini wakitaka uchunguzi huo ufanywe na watu wasiowajibika kwa serikali ya Marekani.

Ricardo Sunga ni mkuu wa jopo hilo.

(Sauti ya Ricardo)

“Tunalaani vikali mwendelezo wa mauaji ya wamarekani weusi; wanaume, wanawake, watoto ikiwemo visa ambavyo hata havitambuliki. Jopo hili la kikazi linashawishika kuwa chanzo cha tatizo hilo ni ukosefu wa dhati wa uwajibikaji wa watekelezaji wa mauaji haya licha ya ushahidi. Tuna wasiwasi zaidi na idadi ndogo ya kesi ambazo zimewajibisha maafisa wa umma.”