Shirika la msalaba mwekundu latoa usaidizi dhidi ya homa ya bonde la ufa Niger.
Shirika la msalaba mwekundu la Niger kwa uratibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, limewatuma wafanyakazi wake 60 wa kujitolea kusambaza taarifa, na ujumbe wa kinga kwa jamii zilizoathiriwa na homa ya bonde la ufa.Taarifa kamili na Amina Hassan.
(Taarifa ya Amina)
Kisa cha kwanza kilibainika katika mkoa wa Tahoua nchini Niger mwezi uliopita lakini hadi sasa ugonjwa huo umesambaa katika vijiji 28 mpakani mwa Mali na Algeria.
Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo, mlipuko huo uliotangaza rasmi Septemba 20, umesababisha vifo vya watu 23, huku wengine 60 wakiwa wameathirika , wengi wa waathirika wakiwa ni wafugaji. Kadhalika kuna ripoti za vifo vya mifugo hususani ngo’mbe, kondoo na ngamia.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Niger linasema linatarajia kuongeza usaidizi ili kuokoa maelfu ya watu dhidhi ya homa ya bonde la ufa.
Homa ya bonde la ufa huambukizwa kwa mgusano na mtu mwenye kirusi na dalili zake ni pamoja na homa, udhaifu mwilini, maumivu ya mgongo na kizunguzungu.