Kipindupindu cha katili maisha Malawi

Watu watatu wamefariki dunia na wengine 196 kurepotiwa kuwa mahtuti hadi katikati ya mwezi huu kufuatia mlipuko wa kipindipindu katika sehemu za kaskazini mwa Malawi.
Tangu mlipuko huo utokee juhudi kadhaa zimekuwa zikifanywa na serikali pamoja na mashirika mengine ya msaada kama vile la afya dunaini la WHO kuweza kukabiliana na mlipuko huo hususan katika wilaya ya Karonga inayopakana na Tanzania.
Nayo ofisi ya Malawi ya WHO, ilifunga safari hadi wilaya hiyo kutathmini hali ya afya.
Msafara wa WHO uligundua miongoni mwa mengine kuwa kamati ya wilaya inayoshughuliia mlipuko huo inasimamiwa na mtu mmoja tu bwana afya wa wilaya hiyo, Dr Phinias Mfume.
Kipindupindu inasemekana kilianzia katika vituo vya afya katika maeneo ya kaskazini na kilikuwa kinasambaa sehemu za kusini.
Ujumbe wa WHO uliweza kushiriki katika mikutano mbalimbali ya kijamii pamoja na viongozi wa vijiji, wanaojitolea pamoja na washirika wanaounga mkono wilaya ya Karonga kuweza kutokomeza ugonjwa huo.
Wote walioshiriki katika mikutano hiyo walikubaliana kuwa chachu ya ugonjwa huo ni uchafu pamoja na maji.
Wasiwasi mwingi kuhusu hali hiyo ni uchafu miongoni mwa jamii za wavuvi kandokando mwa ziwa Malawi. Mmoja wa afisa aliuambia mkutano mmoja kuwa famila nyingi katika sehemu hizo zina nymba za mda tu na bila vyoo na wale walionavyo viko katika hali isioridhisha.
Isitoshe watu hunywa maji ambayo hayakuchemshwa wanayochota kutoka kwenye ziwa ilhali wengine hujisadia katika maji ya ziwa.
Ujumbe wa WHO uliomba afisa wa afya wa wilaya kufanya kila liwezekanalo kuwasiliana na wenzao wa upande wa pili wa mpaka wa Tanzania katika juhudi za kukabiliana na mlipuko huo wa Kipindipindu.